UKAME NA UKOSEFU WA USALAMA WAWAPA WASIWASI WAKAZI WA KACHELIBA.

Na Benson Aswani
Ukosefu wa lishe kwa mifugo umeendelea kuwaathiri mifugo katika Eneobunge la Kacheliba kaunti hii ya poko magharibi huku ukosefu wa amani baina ya jamii ya Pokot na Karamoja ukiwapa wafugaji wasiwasi.
Kwa mujibu wa Solomon Ikwanakoda mkazi wa Naparakocha, Baadhi ya watu wa jamii ya Karamoja wangali wanatumia bunduki licha ya kuwa Rais Museveni alifanya oparesheni ya kuondoa silaha hizo miongoni mwa jamii hizo mbili.
Kumekuwepo na wizi wa ng’ombe ambao umeripotiwa tangu mkataba wa Nablatuk kuondolewa mwezi wa tatu mwaka huu.
Ametoa changamoto kwa viongozi wakuu wa jamii ya Pokot kule Uganda na pia Kenya kushirikiana ili kurejesha amani miongoni mwa jamii hizo mbili.