UJENZI WA SOKO LA SWAM KAUNTI YA TRANS NZOIA WAZINDULIWA RASMI


Kamishina wa kaunti ya trans nzoia Sam Ojwang’ amezindua rasmi ujenzi wa ofisi ya forodha na soko eneo la Swam katika mpaka wa Kenya na Uganda shughuli itakayogharimu takriban shilingi milioni 100.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Ojwang amesema serikali ya rais Uhuru Kenyatta imejitolea kuboresha maisha ya raia wake kwa kutekeleza miradi mikuu ya maendeleo katika kaunti hiyo ya Trans nzoia.
Ni mradi ambao umechangamkiwa pakubwa na wakazi wa eneo hilo la mpakani ambao wamesema kuwa utaleta maendeleo ambayo yatawanufaisha pakubwa mbali na kuhakikisha fedha ambazo wamekuwa wakitumia bidhaa mbali mbali kutoka taifa jirani la Uganda zinafaidi taifa hili.