UJENZI WA MADARASA KATIKA SHULE YA SIKULU TRANS NZOIA WAKAMILIKA.
Ni afueni kwa wanafunzi wa Shule ya msingi na upili ya Sikulu eneo bunge la Saboti Kaunti ya Trans-Nzoia baada ya kukamilika ujenzi wa madarasa 9 kwenye shule hizo kwa ufadhili wa fedha za maendeleo ya maeneo bunge(NGCDF) .
Akihutubu kwenye hafla ya uzinduzi wa madarasa hayo mbunge wa Saboti Caleb Hamisi amewahakikishia wenyeji eneo bunge hilo huduma bora, akisema ujenzi wa mabarasa hayo Utasadia kukidhi hitaji la idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hizo mbili ya msingi na ile ya upili.
Aidha Hamisi amekosoa vikali viongozi waliomtangulia kwa kile alichokitaja kama kutowashughulikia vyema wenyeji wa eneo bunge hilo haswa kimaendeleo na uboreshaji wa miundo msingi katika sekta ya elimu Elimu.