UJENZI WA CHUMBA CHA KUJIFUNGUA CHAZINDULIWA KIMILILI

Serikali ya kaunti ya Bungoma imezindua ujenzi wa chumba cha kujifungua kina mama katika zahanati ya Bituyu eneo bunge la Kimilili.

Kulingana na afisa mkuu katika wizara ya afya kaunti hiyo Patrick Wandili , ni kwamba chumba hicho kitawafaidi wakaazi kutoka eneo hilo hasa kina mama ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta huduma hizo.

Aidha Wandili amesema mradi huo utakaogharimu kima cha shilingi milioni 4.3 utachukua chini ya majuma 16 kukamilika, huku akiishukuru serikali ya kaunti ya Bungoma kwa kuipa sekta ya afya kipau mbele.