UHAMASISHO WATOLEWA KWA KINA MAMA KUHUSU UMUHIMU WA KUJIFUNGULIA HOSPITALINI.


Asilimia kubwa ya kina mama katika kaunti hii ya Pokot magharibi hawajakumbatia wazo la kujifungulia hospitalini.
Haya ni kulingana na mkuu wa kitengo cha afya ya uzazi katika idara ya afya kaunti hii Wilson Ng’aren ambaye amesema hali hii ndiyo imewalazimu kuanzisha uhamasisho maeneo mbali mbali ya kaunti hii miongoni mwa wadau ili kuhakikisha kuwa kina mama wanajifungulia hospitalini.
Ng’aren amesema kuwa kwa kila alfu 100 ya kina mama ambao hujifungulia nyumbani 443 hufariki dunia kila mwaka wakijifungua visa ambavyo amesema kuwa vingekabiliwa iwapo idadi kubwa ya kina mama wangekumbatia wazo la kujifungulia hospitalini.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na muuguzi Julia sipoti ambaye amesema kuwa wanalenga kukutana na wakazi ili kufahamu sababu inayopelekea kina mama wengi kutojifungulia hospitalini ili kutafuta suluhu kwa hali hiyo.