UHABA WA MIUNDO MSINGI WAKUMBA SHULE NYINGI POKOT MAGHARIBI.


Zoezi la kuwasajili wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza linapoendelea, wakuu wa shule mbali mbali wameendelea kulalamikia uhaba wa miundo msingi kukidhi idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule zao.
Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya mseto ya ELCK Chepareria kaunti hii ya pokot magharibi John Cheruo amesema licha ya shule hiyo kutengewa nafasi 200 ya wanafunzi, idadi kubwa ya wanafunzi wameendelea kujitokeza kusajiliwa akitoa wito kwa wizara ya elimu kuangazia swala hilo.
Wakati uo huo Cheruo amelalamikia changamoto ya fedha za matumizi shuleni humo akisema kuwa wengi wa wazazi wanalalamikia ugumu wa maisha kutokana na ukame ambao ulikithiri mwanzoni mwa mwaka huu na kutokuwa katika nafasi ya kupata fedha za kulipia wanao shuleni hivyo kusalia kutegemea fedha za basari.