UHABA WA MIUNDO MSINGI WAHUJUMU USAJILI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA.


Swala la uhaba wa miundo mbinu limejitokeza pakubwa katika shughuli ya usajili wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza katika baadhi ya shule za kaunti hii ya Pokot magharibi.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya St Bakhita Grace Akure huenda shule hiyo ikakosa kuwachukua wanafunzi wote 195 ambao shule hiyo ilitengewa kutokana na uchache wa madarasa pamoja na mabweni.
Aidha Akure amesema japo shule hiyo imefanya juhudi kuweka mikakati ya kukabili maambukizi ya virusi vya corona miongoni mwa wanafunzi, uhaba wa miundo msingi umesalia changamoto katika kuhakikisha kuwa hitaji la umbali kutoka kwa mwanafunzi mmoja hadi mwingine linazingatiwa.