UHABA WA CHAKULA WATISHIA MASOMO BARINGO.

Na Benson Aswani
Huenda baadhi ya wanafunzi kutoka familia maskini katika kaunti ya Baringo wakalazimika kusitisha masomo yao kutokana na ukosefu wa chakula nyumbani mwao.
Kulingana na mwakilishi wadi ya Bartabwa Ruben Chepsongol tayari baadhi ya wanafunzi wameripotiwa kutoenda shuleni kwa kukosa chakula.
Chepsongol ambaye pia ni kiranja wa wengi kwenye bunge la kaunti ya Baringo sasa anaitaka serikali kuu kusambazia chakula cha msaada wakazi ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaendelea na masomo yao.
Kwa upande mwingine chepsongol ameitaka serikali kuimarisha usalama katika eneo la bonde la kerio kwa kuwakabili wezi wa mifugo wanaendeleza uvamizi na pia mauaji ya watu.