UGEMAJI POMBE WAIBUA WASIWASI KUHUSU HATIMA YA VIJANA BARINGO KASKAZINI.

Na Benson Aswani
Wasomi katika eneo bunge la Baringo kaskazini kwenye kaunti ya Baringo sasa wanawataka maafisa wa usalama kuanzisha msako mkali wa kuwakabili wagemaji na wauzaji wa pombe haramu.
Wakiongizwa na daktari Wilson Kiptala ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha moi mjini Eldoret wamesema kwamba kwenye baadhi ya maeneo kama vile westgate watu na hususan vijana hubugia pombe kuanzia alfajiri hadi usiku wa manane.
Kiptala ameongeza kuwa licha ya vijana kusoma na hata kufuzu katika vyuo vikuu wengi wao wamekosa kazi hali ambayo anasema huenda ndio imewafanya kuwa waraibu wa mihadarati.
Kiptala ambaye pia analenga kuwania kiti cha ubunge eneo hilo kupitia chama cha UDA aidha ameelezea haja ya viongozi kushirikiana kwa pamoja ili kuwasaidia vijana kupata kazi au kuanzisha miradi itakayowawezesha kupata fedha za kujimudu kimaisha.