UGAVI WA FEDHA ZA MAENDELEO KATIKA SHULE UNAPASWA KUZINGATIA UWAZI WA SHULE.


Mbunge wa Kapenguria kaunti hii ya Pokot Magharibi Samwel Moroto ametoa wito kwa idara ya elimu kaunti hii kutoa fedha kwa shule mbali mbali kwa kuzingatia uwazi wa shule hizo katika matumizi ya mgao huo wa fedha na pia kulingana na jinsi zinavyofanya katika mitihani ya kitaifa.
Kulingana na Moroto ni kwamba zipo baadhi ya shule katika kaunti hii hasa eneo bunge la Kapenguria ambazo zimetekeleza mengi kutokana na fedha zinazopewa ila zinatengewa fedha kidogo sana huku zile ambazo hazizingatii uwazi katika matumizi ya fedha hizo zikitengewa mgao mkubwa wa fedha.
Wakati uo huo Moroto ameshutumu wizara ya elimu katika kaunti hii kwa kufumbia macho vilio vya wazazi kuhusu hali duni ya miundo msingi ya baadhi ya shule maeneo mbali mbali ya kaunti hii huku akidai huenda maafisa katika wizara hiyo wanashirikiana na wakuu wa shule hizo kufuja fedha zinazonuiwa kutekelea maenedeleo.