UFISADI WATAJWA KUWA KIKWAZO KIKUU KWA UKUAJI WA UCHUMI POKOT MAGHARIBI.


Mwaniaji kiti cha mwakilishi kina mama katika kaunti hii ya Pokot magharibi kupitia chama cha KANU Bi. Catherine Mukenyang amesema kuwa utawala wake utatoa kipau mbele kwa vita dhidi ya ufisadi.
Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki mapema jana, Mukenyang alisema kuwa ufisadi umelemeza uchumi wa taifa hili hali ambayo imepelekea umasikini miongoni mwa wakenya, vijana wengi wakisalia bila ajira.
Aidha Bi. Mukenyang alizisuta idara za kukabili ufisadi nchini kwa kutochukua hatua dhidi ya wanaopatikana kuhusika ufisadi hali ambayo imepelekea kukithiri wizi wa fedha za umma.
Wakati uo huo aliahidi kubuni idara ya vijana na michezo katika afisi yake lengo kuu likiwa kukuza vipaji miongoni mwa vijana akiwahakikishia wakazi kuwa atahakikisha anatekeleza yote anayoahidi iwapo atatwaa kiti hicho.