UDA YATAKIWA KUTOJIPIGA KIFUA KUFUATIA USHIONDI WA KIAMBAA.


Ushindi wa mwaniaji wa UDA katika uchaguzi mdogo wa ubunge eneo la Kiambaa hauashirii chochote kuhusu umaarufu wa UDA maeneo mbali mbali nchini.
Haya ni kwa mujibu wa seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio ambaye amesema kuwa UDA ni moja ya vyama tanzu vya Jubilee akiongeza kuwa chaguzi ndogo haziwezi kuwa kipimo cha umaarufu wa chama.
Poghisio amewataka wanachama wa chama hicho kinachohusishwa na naibu rais William Ruto kutojipiga kifua kufuatia ushindi huo kwani wapiga kura walioshiriki uchaguzi huo hawakufanya hivyo kutokana na chama bali kwa mtu waliyempendelea, ikizingatiwa mshindi wa kiti hicho alikuwa mwanachama wa Jubilee kabla ya kujiunga na UDA.
Wakati ou huo poghisio amepuuzilia mbali mipango ya kubuniwa chama kipya kaunti hii akisema gavana John Lonyangapuo anafaa kutumia juhudi hizo kuhakikisha anatekeleza maswala ya kumfaidi mkazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi.