UDA YAANZA MIKAKATI YA KUTEKELEZA MFUMO WA UCHUMI WA BOTTOM UP POKOT MAGHARIBI.


Viongozi wa chama cha UDA kinachoongozwa na naibu rais William Ruto katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameanza mikakati ya kuangazia mikakati ya jinsi ya kutekeleza matakwa ya wananchi iwapo chama hicho kitatwa uongozi wa taifa baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza baada ya kukutana na viongozi hao mwanachama wa kamati ya kampeni ya naibu rais William Ruto Prof. Edward kisiang’ani amesema kuwa uongozi wa chama cha UDA utaangazia zaidi yale ambayo mwananchi wa kiwango cha chini anahitaji wala si malengo yake iwapo itachaguliwa kuongoza serikali ijayo, kwani chama hicho hakina ajenda yake bali ile ya mwananchi.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na mwakilishi wadi maalum Elijah Kasheusheu ambaye amesema hatua hiyo itasaidia pagubwa katika kuweka mikakati ya jinsi ya kuwainua kiuchumi wananchi wa hali ya chini kupitia mfumo wa kiuchumi wa bottom up economic Model unaishinikizwa na chama cha UDA.
Kwa upande wake mgombea kiti cha ubunge eneo la pokot kusini Joel Arumonya amesema kuwa mfumo wa kiuchumi wa naibu rais William Ruto utasaidia pakubwa kusuluhisha matatizo yanayowakumba wakazi wa kaunti hii anaosema kuwa asilimia kubwa wanaishi katika hali a umasikini.