‘UDA KINGALI CHAMA TANZU CHA JUBILEE’ ASEMA MOROTO.


Mbunge wa kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto amekanusha madai kuwa baadhi ya wendani wa naibu rais William Ruto wanapanga kususia mkutano wa chama cha jubilee unaotarajiwa ili kupanga mikakati ya uchaguzi wa chama hicho mashinani.
Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki Moroto amesema kuwa licha ya kujihusisha na chama cha UDA wangali wanachama wa jubilee kwani chama hicho ni moja ya vyama tanzu vya jubilee.
Moroto amesema kuwa wendani wa naibu rais walilazimika kuanza kujihusisha kikamilifu na chama cha uda baada ya kutengwa katika shughuli za chama tawala cha jubilee.