UDA CHAENDELEA KUJIUZA POKOT MAGHARIBI.


Baadhi ya viongozi katika kaunti ya Pokot magharibi wanachama wa chama cha UDA ambacho kinahusishwa na naibu rais William Ruto wamendelea kukipigia debe chama hicho kwa lengo la kukiuza mashinani.
Julius Murgor ambaye ametangaza kugombea kiti cha useneta kaunti ya Pokot magharibi katika uchaguzi mkuu ujao amewataka wakazi wa kaunti hii kukiunga mkono chama hicho kutokana na hali kuwa kinaangazia zaidi kuinua viwango vya maisha ya mkenya wa kawaida.
Wakati uo huo Murgor amepuuzilia mbali madai ya kubuniwa chama kipya katika kaunti hii kwa jina Mtelo akisema hamna mkutano wowote ambao umeandaliwa na viongozi wa kaunti hii ili kubuni chama hicho akiyataja madai hayo kuwa uvumi.