UCHUNGUZI WAANZISHWA KUHUSU UTATA UNAOZINGIRA KIFO CHA KANGOGO.


Makachero wa idara ya upelelezi wa jinai DCI kwenye kitengo cha kuchunguza mauaji wametumwa katika kaunti ya Elgeyo marakwet kuchunguza kifo cha afisa wa polisi mwanamke Caroline Kangogo.
Kifo chake Kangogo mwenye umri wa miaka thelathini na minne anayetuhumiwa kuwaua wanaumme wawili, mmoja akiwa ni polisi kilifikisha mwisho siku kumi mfululizo za kumtafta.
Licha ya polisi kudai kwamba polisi huyo alijiua maswali yameibuka kuhusu kifo chake baada ya watu kutilia shaka dhana kwamba alijiua.
Kangogo alipatikana ameaga dunia ndani ya boma la wazazi wake katika eneo la Nyawa kule Elgeyo marakwet akiwa na bastola mkononi huku mwili ukiwa umeloa damu.
Makachero wa DCI pia wamesema kwamba wanachunguza jumbe ambazo polisi wanadai kangogo aliandika kabla ya kujiua
Katika jumbe hizo kangogo analaumu msukosuko kwenye ndoa yake kutokana na masaibu yake akidai familia yake ilimsikiza mume wake tu bila kusikiliza upande wake.