UCHUNGUZI UNATARAJIWA KUFANYIKA KATIKA TAIFA JIRANI LA UGANDA NA KENYA MPAKANI MWA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUHUSIANA NA MADAI YA UFISADI.
Idara za uchunguzi katika wilaya ya Amudat mipakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na taifa jirani la Uganda zinatarajiwa kuendesha uchunguzi kuhusu visa kadhaa vya ufisadi.
Akizungumza na wanahabari katika hafla ya maadhimisho ya siku ya akina mama yaliyochelewa kuadhimishwa katika wilaya hiyo RDC wa eneo hilo Michael Bwalatum amesema kuwa makundi ya akina mama ndiyo yaliyoathirika zaidi katika visa hivyo.
Amesema kuwa vingi vya visa hivyo viliteketelezwa katika utawala uliotangulia ambapo maafisa kadhaa hasa waliokuwa wakisimamia maswala ya fedha wanachunguzwa na watachukuliwa hatua wakipatikana na makosa.