UAMUZI WA RAIS KUONGEZA KAFYU KWA SIKU 60 WAKASHIFIWA VIKALI


Baadhi ya wafanya biashara mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu wamekosoa hatua ya serikali kuongeza mda wa kutekeleza marufuku ya kafyu kwa siku 60 zaidi kuanzia tarehe 28 mwezi mei.
Wafanya biashara hao wanasema kuwa kuongezwa mda huo kutawaathiri zaidi na hata kupelekea kusambaratika kabisa biashara zao.
Wameongeza kuwa tangu serikali ilipotangaza marufuku hayo kwa lengo la kukabili janga la virusi vya korona mapato yao yameshuka huku baadhi wakilazimika kufunga shughuli zao.
Kulingana na wafanya biashra hao, serikali inastahili kuondoa marufuku hayo au kusongeza mda wa kuanza kutekelezwa masharti ya kafyu kutoka saa nne hadi saa tano usiku.
Katika tangazo kwenye gazeti rasmi la serikali ijumaa wiki iliyopita, waziri wa usalama wa ndani Dr. Fred Matiang’i alisema kuwa marufuku ya kutokua nje kuanzi saa nne hadi saa kumi alfajiri yaliyokua yatamatike tarehe 29 yataendelea kutekelezwa kwa siku 60 zaidi.