UAMUZI WA KUTUPILIA MBALI MCHAKATO WA BBI WAENDEELA KUPONGEZWA

Uamuzi wa majaji watano wa mahakama kuu walioharamisha mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho kupitia mswada wa BBI umeendelea kupongezwa wa hivi punde wakiwa ni viongozi kutoka kaunti ya Baringo.

Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Mogotio Charles Koskei, viongozi hao wamesema kuwa uamuzi wa majaji hao ulizingatia sheria ambapo amewahimiza viongozi na wakenya kuheshimu uamuzi huo.

Kosgei ametetea hatua ya bunge la kaunti ya Baringo kuuangusha mswada huo akisema kwamba walibaini kuwa haukuwa umebuniwa kulingana na sheria.