‘TUSINYAKUE ARDHI KIMABAVU’ ASEMA MWAKILISHI WADI YA MNAGEI BENJAMIN ARAULE


Mwakilishi wadi ya Mnagei kaunti hii ya Pokot Magharibi Benjamin Araule ameshutumu hatua ya mkazi mmoja eneo la Psigirio katika wadi ya Mnagei kunyakua barabara ya umma anayodai iko katika ardhi yake.
Akizungumza wakati wa shughuli ya kurejesha sehemu ya barabara hiyo, Araule ametoa wito kwa wakazi kufuata njia za kisheria katika kudai ardhi wanazohisi kuwa ni zao na wala si kuzinyakua kwa mabavu.
Msimamizi wa wadi ya Mnagei Meshack Kakuko kwa upande wake amesema licha ya saveya wa kaunti pamoja na kaunti kamishina kuthibitisha kuwa sehemu hiyo ya barabara ni ya umma, jamaa huyo amezidi kuinyakua, huku akitoa wito wa hatua kuchukuliwa ili hali hiyo isishuhudiwe tena.
Ni swala ambalo idara ya polisi kupitia OCS wa Kapenguria Wamocha Wechape imesema kuwa watafuatilia, huku akitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo walio katika ardhi ya barabara ya kutoka Kitale hadi Morpus kuondoka kabla ya kuanza ukarabati wa barabara hiyo.