TUME YA UCHAGUZI IEBC WATAKIWA KUBATILISHA HITAJI LA VYETI VYA MASOMO KATIKA KUWANIA VITI VYA KISIASA.


Baadhi ya wagombea wa viti mbali mbali vya kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu sasa wanaitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kubatilisha hitaji la vyeti vya masomo kwa wagombea wa nyadhifa za uongozi.
Akizumza na kituo hiki mgombea kiti cha ugavana katika kaunti ya Trans nzoia Mary Maria amesema kuwa kila mgombea wa kiti cha kisiasa anastahili kupewa fursa hiyo bila kujali viwango vya elimu kwani uongozi bora hautegemei elimu ya mtu na kuwa wapo viongozi wengi ambao hawana vyeti hivyo ila utendakazi wao ni wa kupigiwa mfano.
Maria ambaye ametangaza kugombea kiti hicho kwa tiketi ya chama cha UDA, amewataka wakazi wa kaunti hiyo kumpa fursa ya kuwaongoza akiahidi kuwa uongozi wake utatoa kipau mbele kwa mkenya wa kipato cha chini ili kuhakikisha uchumi wake unaimarishwa, kando na kuhakikisha hali ya mji wa kitale unaimarishwa.