TSC YATAKIWA KUAJIRI WALIMU ZAIDI KWA SHULE ZA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Tume ya huduma kwa walimu TSC imetakiwa kuhakikisha walimu zaidi wanatumwa katika shule za kaunti hii ili kuiwezesha kuwa katika nafasi bora ya kutoa ushindani unaostahili na kuwa sawa na shule zingine kote nchini
Mbunge wa Sigor Peter Lochakapong amesema shule nyingi katika kaunti hii zilikosa kufanya vyema katika baadhi ya mosomo kwenye mitihani ya kitaifa mwaka huu kutokana na uchache wa walimu ambao wanafunza masomo hayo.
Wakati uo huo Lochakapong amerejelea wito wake kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kuhakikisha kuwa wanawapeleka wanao shuleni ili wapate elimu kama watoto wengine nchini, hasa wakati huu ambapo kunashuhudiwa amani kaunti hii.