TRANS NZOIA YASAJILI ASILIMIA 32 YA WAPIGA KURA.


Asilimia 68 ya wapiga kura waliolengwa kusajiliwa kuwa wapiga kura wapya katika kaunti ya Trans nzoia kwenye zoezi la usajili wa wapiga kura wapya ambalo lilikamilika tarehe 6 mwezi huu hawakujitokeza kufanya hivyo.
Afisa wa tume ya uchaguzi IEBC katika kaunti hiyo Lazarus Chebii amesema licha ya asilimia kubwa ya vijana kuhamasishwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwemo kufanya mikutano vijijini, kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii asilimia iliyojitokeza ni 32 pekee.
Hata hivyo chebii amewasihi wale walioachwa, kujitokeza katika afisi za IEBC katika maeneo bunge kusajiliwa kabla ya tarehe 28 mwezi huu wakati ambapo shughuli hiyo sasa itafungwa rasmi katika afisi za IEBC.