TRANS NZOIA YAPOKEA DAWA ZA KIMA CHA SHILINGI M 54.7 KUTOKA KEMSA.


Ni afueni kwa wenyeji wa Kaunti ya Trans Nzoia baada ya kaunti hiyo kupokea dawa za kima cha shilingi Milioni 54.7 kutoka mamlaka ya usambazaji dawa na vifaa vya matibabu nchini KEMSA.
Akihutubu baada ya kupokea dawa hizo, Naibu Gavana Kaunti ya Trans Nzoia Dkt Stanley Tarus amesema Serikali yake itahakikisha dawa hizo zinafikia vituo vyote vya afya mbali na kuhakikisha kwamba zinatumika vyema.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na waziri wa Afya Kaunti ya Trans Nzoia Claire Wanyama ambaye aidha amehimiza wenyeji Kaunti hiyo kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.