TRANS NZOIA YAPIGWA JEKI KATIKA UHIFADHI WA MSITU WA MLIMA ELGON
Na Benson Aswani
Kaunti ya Trans-Nzoia ni miongoni mwa Kaunti zinazotazamia ufadhili wa shilingi Dola Milioni 6 ya utunzaji wa msitu wa Mlima elgon kupitia wa ufadhili wa ushirkia wa maendeleo FAO.
Akihutubu baada ya mkutuno uliowaleta pamoja washikadau katika sekta ya mazingira ikiwa ni pamoja na wizara ya kilimo na ile ya misitu waziri wa mazingira Kaunti ya Trans-Nzoia Andrew Musungu amesema wizara yake pia itatenga fedha kwa mradi huo lakini ufadhili mkubwa unatoka kwa wafadhili.
Aidha Musungu amesema wizara yake imeweka mikakati mbali na kupasisha sheria itakayowezesha uhifadhi wa msitu huo, na jinsi gani wataweza kuhusisha umma katika utunzaji wa miti itakayopandwa chini ya mradi huo ili kuafikia malengo yao.