TRANS NZOIA YANUFAIKA NA UFADHILI CHINI YA MPANGO WA GEAP.

Kaunti Trans-nzoia ni miongoni mwa kaunti 12 zitakazo faidi ufadhili wa kifedha wa kima cha zaidi ya shilingi bilioni 1.2 kutoka kwa serikali ya Denmark chini ya mradi wa Green Employment Agriculture Programme GEAP na kutekelezwa na Micro Enterprise Support Programme Trust ili kupiga jeki sekta nne za uzalishaji wa kilimo ikiwa ni pamoja na ukuzaji wa samaki, uzalishaji wa maziwa, ufugaji wa kuku wa kienyeji pamoja na kilimo cha parachichi.

Akihutubu kwenye warsha ya kuhamasisha maafisa wakilimo nyanjani uliofadhiliwa na mradio huo, waziri wa kilimo kaunti ya Trans-nzoia Mary Nzomo amesema mradi huo utakuwa wa manufaa kwa wakulima kaunti hiyo kwani utasadia kupiga jeki uzalishaji wa chakula, kuimarisha uchumi na lishe bora kwa jamii.

Aidha Nzomo amesema mradi huo unatilia maanani kuhusishwa akina mama na vijana katika kuimarisha shughuli za kilimo na uzalishaji mbali na kuwasaidia kupata fedha za kufadhili miradi yao ya maendeleo.

Kwa upande wake mshirikishi wa shirika la GEAP Jerald Ochieng amesema mradi huo unalenga kutafuta soko kwa bidhaa za kilimo ufadhili wa kifedha kwa wakulima,usalama na uzalishaji wa chakula na uimarishaji wa mazingira.