TAHARUKI YAENDELEA KUTANDA CHESOGON MPAKANI PA POKOT MAGHARIBI NA ELGEYO MARAKWET.


Baadhi ya viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameilaumu pakubwa serikali kwa kushindwa kudhibiti usalama katika eneo la Chesogon mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet.
Wakizungumza baada ya kuzuru eneo ambako raia wanne waliuliwa majuzi, viongozi hao wakiongozwa na mbunge wa Sigor Peter Lochakapong wanasema kuwa huenda masomo yakaathirika pakubwa, wakati uo huo wakitaka familia zilizopoteza wapendwa wao kupewa fidia.
Inaarifiwa nne hao waliuliwa kwa kupigwa risasi na wavamizi wanaoshukuwa kutoka kaunti jirani hali ya taharuki ikiendelea kushuhudiwa eneo hilo huku vijiji vikisalia mahame baada ya wakaazi kuhamia maeneo salama kwa kuhofia usalama wao.
Hayo yanajiri huku polisi katika eneo hilo wakiendeleza oparesheni ili kuwanasa washukiwa.