TAHADHARI YATOLEWA KWA WANAFUNZI WAKAIDI KAUNTI NDOGO YA KAPENGURIA.
Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Julius Kyumbule, amelalamikia ongezeko la migomo shuleni katika siku za hivi karibuni.
Kyumbule amesema kuwa katika siku za hivi karibuni kumeripotiwa visa kadhaa vya utovu wa nidhamu miongoniu mwa wanafunzi ikiwemo majaribio ya kuteketeza mabweni ya shule akisema baadhi ya wanafunzi wanaoshiriki uovu huo tayari wamekamatwa na watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Kyumbule ametoa wito kwa wadau kuhakikisha wanatoa miongozo kwa wanafunzi dhidi ya kuhisika visa vya utovu wa nidhamu kwani sheria i wazi na itamwandama kila anayehusika uovu wowote shuleni.
Wakati uo huo Kyumbule amewataka wakuu wa shule pamoja na kamati katika shule hizo kubaini vyanzo vya migomo ya mara kwa mara shuleni ili kuweka mikakati ya kukabili visa hivyo.