TAHADHARI YATOLEWA KWA WAKAZI POKOT MAGHARIBI KUHUSU KUUZIWA PLOTI.


Wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wametahadharishwa dhidi ya kuhadaiwa na watu wanaodai kuwa maafisa kutoka wizara ya ardhi ili kukatiwa ploti katika miji na vituo vya kibiashara ambako kunafanyika shughuli ya mipangilio ya miji.
Afisa mkuu katika wizara ya ardhi na mipangilio ya miji katika kaunti hii ya Pokot magharibi Ibrahim Long’olomoi amesema kuwa wapo baadhi ya wakazi ambao wamelaghaiwa fedha zao na watu wa sampuli hiyo kwa madai ya kukatiwa ploti katika miji ambako shughuli hiyo inaendelea.
Long’olomoi amewataka wakazi kuwa makini na kutojikuta katika mtego huo akisema kuwa maafisa kutoka wizara ya ardhi hawafanyi kazi ya kugawa ploti katika miji bali shughuli hiyo hutekelezwa na maafisa wa mipangilio ya miji wa kaunti.