SWALA LA ARDHI LAZIDI KUIBUA UTATA TRANS NZOIA.


Viongozi kutoka Kaunti ya Trans Nzoia sasa wanataka shughuli ya kurejesha ardhi yote ya umma iliyonyakuliwa na watu binafsi kutekelezwa kwenye ardhi zote za umma haswa mjini Kitale, wakisema asilimia 80 ya ardhi ya umma Kaunti hiyo imenyakuliwa.
Wakiongozwa na Richard Kamonda Chesebe viongozi hao wanadai kulenga baadhi ya wanyakuzi hakutatoa suluhu kwa suala la unyakuzi wa mali ya umma akimtaka Seneta wa Kaunti ya Trans Nzoia Michael Mbito na kamati ya seneti ya ardhi kuorodhesha ardhi zote za umma zilizonyakuliwa na mabwenyenye na kuzirejesha kwa serikali.
Aidha Chesebe ametaka wafanyabishara waliofurushwa kwenye ardhi ya reli kutafutiwa sehemu mbadala ya kufanyia bishara zao ili kupunguza msongamano mkubwa unaoshuhudiwa kwa sasa katikati ya mji wa Kitale.