SPIKA WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI ASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE NA WANAWAKE KUTOKA KAUNTI TOFAUTI


Huku dunia nzima ikiadhimisha siku ya wanawake, spika wa kaunti ya Pokot Magharibi Catherine Mukenyang’ amewaongoza wanawake kutoka kwenye kaunti za Pokot Magharibi, Turkana, Elgeiyo Marakwet na Trans-Nzoia kwenye kongamano lililochukua siku tatu mjini Makutano kwenye kaunti hii ya Pokot Magharibi.
Mkutano huo wa makundi ya wanawake yakiwemo ya watu wenye ulemavu kwa ushirikiano na shirika la msalaba mwekundu na muungano wa kitaifa wa biashara na viwanda umefisha kilele leo hii huku kaulimbiu ya siku hii ikiwa ni ‘Choose to Challenge’.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mukenyang’ amesema japo kuna vizingiti vinavyozuia ukuaji wa biashara hasa suala la utamaduni, wanawake wanafaa kutafuta mbinu ya kujikwamua navyo ili kupiga hatua mbele zaidi kwenye biashara zao.