SPIKA WA BUNGE WA POKOT MAGHARIBI AHIDI KUFANYA VYEMA KATIKA KULIONGOZA BUNGE


Spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Fredrick Kaptui amesisitiza kujitolea kwake kuhakikisha kwamba wabunge katika bunge la tatu la kaunti hii wanafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano kuhakikisha kwamba wananchi wanpata huduma bora.
Akizungumza baada ya kuapishwa spika wa bunge hilo, Kaptui aidha amesema kwamba bunge hilo litashirikiana na serikali tendaji ikiwemo kubuni sheria zitakazohakikisha kwamba mwananchi wa kawaida ananufaika litakapoanza rasmi vikao vyake tarehe 4 mwezi Octoba.
Aliyekuwa mshindani wake katika kinyang’anyiro hicho wakili Philip magal amepongeza jinsi shughuli hiyo ilivyoandaliwa akisema kuwa ilikuwa huru na haki na hamna aliyependelewa huku akimtakia heri njema spika Kaptui.
Katibu wa bunge hilo Benedict Toroitich ametumia fursa hiyo kuwapongeza wote walioshiriki katika juhudi za kufanikisha shughuli hiyo ambayo ameitaja kuwa iliyofana.

[wp_radio_player]