SPIKA WA BUNGE LA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI CATHERINE MUKENYANG’ ASEMA HANA NIA YA KUMBANDUA MAMLAKANI GAVANA LONYANG’APUO

POKOT MAGHARIBI


Spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot Magharibi Catherine Mukenyang amesema kuwa hana nia yoyote ya kumbandua gavana wa kaunty hii ya Pokot Magharibi John Lonyangapuo.
Kwenye mahojiano ya kipekee ndani ya mpigo wa Kalya Radio mapema leo, spika Mukenyang amesema kwamba iwapo hoja hiyo ya kumtimua gavana Lonyangapuo uongozini itawasilishwa bungeni yeye kama refari wa bunge ataipokea na kuisikiliza hoja hiyo ila kwa sasa hana nia kama hiyo.
Spika Mkenyang aidha amesema kwamba ni vyema viongozi kuongoza bila ya kuwasikiliza wahuni fulani katika kukandamiza uongozi wao.