SPIKA WA BUNGE LA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AWASILISHA MAKARATASI YAKE KATIKA OFISI YA IEBC


Mwaniaji wa kiti cha mwakilishi kina mama katika kaunti hii ya Pokot magharibi ambaye ni spika wa bunge la kaunti hii Catherine Mukenyang ameidhinishwa rasmi kuwania kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.

Ni afisa wa uchaguzi wa tume ya IEBC kaunti hii ya Pokot magharibi Joyce Wamalwa akimwidhinisha rasmi mgombea kiti cha mwakilishi kina mama katika kaunti hii Catherine Mukenyang.

Akizungumza baada ya kuidhinishwa rasmi , Mukenyang amesema kuwa atayapa kipau mbele maswala ya kuwawezesha kina mama kupitia sacco za kibiashara, watu wanaoishi na ulemavu ambapo amesema atahakikisha kila mlemavu anapokea matibabu ya bure.

Aidha Mukenyang amesema kuwa atabuni vituo vya kubaini vipawa miongoni mwa vijana katika kila maeneo bunge na wadi.

Wakati uo huo Mukenyang ametoa wito kwa wagombea wote wa nyadhifa za kisiasa kuendesha kampeni zao kwa njia ya amani, huku pia akiwataka vijana katika kaunti hii kutokubali kutumika na wanasiasa kuvuruga amani taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

[wp_radio_player]