SPIKA WA BUNGE LA KAUNTI YA POKOT AZUILIWA KUINGIA AFISINI MWAKE NA WAWAWKILISHI WADI WA BUNGE HILO LA POKOT


Na Benson Aswani
Kwa mara nyingine spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Catherine Mukenyang amezuiwa kuingia katika bunge hilo kuongoza vikao kufuatia hatua ya bunge hilo kumbandua afisini tarehe 7 mwezi septemba mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari mapema leo Mukenyang amedai kufungiwa lango la makao ya bunge wafanyikazi wa kaunti wakitumwa kumzuia kuingia licha ya agizo la mahakama la kumtaka kuendelea na shughuli zake hadi itakaposikilizwa na kuamuliwa kesi aliyowasilisha kupinga kubanduliwa kwake.
Mukenyang ameelezea hofu kuwa huenda bunge hilo likachukuliwa hatua kwa kufeli kutekeleza jukumu la kuchunga mali ya umma kufuatia malumbano yanayoshuhudiwa baina ya spika na bunge hilo, huku akitishia kufika mahakamani kwa madai ya kushambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wa kaunti.