SIMON KACHAPIN ATEULIWA KUHUDUMU KAMA KATIBU KATIKA WIZARA YA MICHEZO NA UTAMADUNI


Katibu katika wizara ya michezo na utamaduni Simon Kachapin amempongeza rais Uhuru Kenyatta kwa kumteua kuhudumu katika wizara hiyo mpya.
Kachapin ambaye awali alihudumu katika wizara ya kawi, amemhakikishia rais kuwa atatekeleza majukumu yake inavyostahili na kumsaidia kupitia michezo na utamaduni kuhakikisha anaacha taifa lenye umoja wakati akistaafu baada ya kukamilisha kipindi chake cha kuhudumu.
Aidha kachapin amesema atashirikiana na wadau mbalimbali kuimarisha vipawa miongoni mwa vijana nchini kupitia michezo mbalimbali ikiwa moja ya malengo ya mtaala mpya wa elimu wa CBC.
Wakati ou huo Kachapin ameahidi kushirikiana na serikali ya kaunti hii ya Pokot Magharibi katika kuimarisha hali ya uwanja wa michezo wa Makutano ikiwa ni moja ya miradi anayopanga kutekeleza katika kaunti hii katika kipindi ambacho anatarajiwa kuhudumu kwenye wizara hiyo.