SIASA ZAPIGWA MARUFUKU MAKANISANI POKOT MAGHARIBI.

Na Benson Aswani
Viongozi wa kidini katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamekubaliana kwa kauli moja kutoruhusu viongozi wa kisiasa kuendeleza kampeni zao katika maeneo ya kuabudu.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari baada ya kikao kilichohusisha viongozi wa dini ya kikristo na wale wa kiislamu, viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti mshirikishi wa baraza la makanisa NCCK tawi la Pokot magharibi Moses Longiro wamesema kuwa makanisa ni maeneo ya kuabudu hivyo siasa zinapasa kuendeshwa nje ya maabadi.
Hata hivyo viongozi hao wamesema kuwa hawajawapiga marufuku wanasiasa kuhudhuria ibaada za kawaida makanisani.
Aidha viongozi hao wametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuhubiri amani wanapoendeleza kampeni zao kwa jili ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao pamoja na kutii sheria ili kuzuia kushuhudiwa vurugfu nchini jinsi ilivyoshuhudiwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mshirikishi wa baraza la waislamu Supkem kanda ya kasakazini mwa bonde la ufa haji Omar Jumbe ambaye pia amewataka vijana kutokubali kutumika na wanasiasa kuzua vurugu katika mikutano mbali mbali ya kisiasa.