SIASA ZAPIGWA MARUFUKU KATIKA HAFLA ZA MAZISHI KIMAETI BUNGOMA.


Chifu wa kata ya Kimaeti eneo bunge Bumula kaunti ya Bungoma Siafu Fwamba amepiga marufuku wanasiasa kupewa nafasi ya kuzungumza katika hafla za mazishi katika kata yake .
Fwamba amesema kuwa amechukua hatua hiyo ili kuwazuia wanasiasa hao ambao wamekuwa na mazoea ya kuwakusanya wakazi wengi kukaidi masharti ya wizara ya afya ya kukabili msambao wa virusi vya corona huku wakitumia mikutano hiyo kueneza sera zao na kuendeleza machafuko ya kisiasa.
Fwamba sasa ametoa wito kwa machifu wenzake katika kaunti ya Bungoma kuiga mfano huo ili kuokoa maisha ya wakenya hasa kikizingatiwa kuwa wanafunzi wanajiandaa kufunga shule wiki hii.