SIASA ZA MAZISHINI ZAPIGWA MARUFUKU POKOT MAGHARIBI.


Gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi Prof John Longanyangápuo amepiga marufuku siasa katika hafla za mazishi katika Kaunti hii akitaka wanasiasa kuheshimu familia za waliofiwa.
Akihutubu kwenye hafla ya mazishi ya aliyekuwa kiongozi mkuu wa jamii ya Sengwer /Cherangany Moses Leleu Laima eneo la Talau eneo bunge la Kapenguria Lonyangapuo ametaka wanaotaka kuwania viti mbalimbali kutengeneza hafla zao na kukoma kubadili hafla za mazishi kuwa majukwaa ya kisiasa.
Adha Lonyangapuo amewahimiza wenyeji wa Kaunti hii kuwa na subira wanapojipanga kuhusu watakaomuunga mkono kwenye siasa za mwaka wa 2022, akisema yeyote anayetaka kuungwa mkono na jamii hii ni sharti kuweka wazi ajenda yake kwa Jamii na Kaunti ya Pokot Magharibi.
Lonyangapuo ameahidi kusaidia jamii hiyo kupitia kwa wakfu Wa Sengwer/Cherangany kama njia moja wapo ya kuinua maisha ya jamii hiyo ya walio wachache kutoka Kaunti za Pokot magharibi,Trans Nzoia na Elgeiyo Marakwet.