‘SI WAKATI WA KULEGEZA MASHARTI YA KUKABILI COVID 19,’ ASEMA APAKORENG.

Na Benson Aswani
Wito umetolewa kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kutolegeza kamba katika kuzingatia masharti ya kukabili maambukizi ya virusi vya corona licha ya takwimu kuonyesha kupungua maambukizi ya virusi hivyo humu nchini.
Waziri wa afya kaunti hii Christine Apakoreng amesema kuwa licha ya kupungua maambukizi haya, virusi vya corona vingalipo na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa anapokea chanjo dhidi ya covid 19 ili kujihakikishia kinga dhabiti ya mwili dhidi ya ugonjwa huo.
Amesema kuwa hadi kufikia sasa kaunti hii imewachanja zaidi ya wakazi alfu 4 idadi anayosema kuwa si ya kuridhisha kulingana na viwango hitajika vya shirika la afya duniani WHO vya asilimia 40 ya waliochanjwa kitaifa ili kuhakikisha kinga kamili itakayopelekea kurejelewa hali ya kawaida.