SHULE YA TABADAN ACADEMY YASIFIWA KWA KUWAHUDUMIA WAATHIRIWA WA DHULUMA ZA JINSIA

Wazazi wametakiwa kutowaondoa wanao katika shule ya msingi ya Tabadan academy iliyoko eneo la Kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi na badala yake kuhakikisha wanafunzi zaidi wanajiunga na shule hiyo.

Ni wito wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Moses Wanyangu ambaye amesema kuwa matokeo bora ambayo yaliandikishwa na shule hiyo katika mtihani wa KCPE ni dhihirisho kuwa hiyo ni shule bora kwa wanao.

Ni kauli ambayo imesisitizwa na OCS wa kituo cha polisi cha Kacheliba Tom Nyanaro ambaye amesema kuwa shule hiyo imekuwa ya manufaa zaidi hasa kwa kuwahudumia watoto ambao wanaokolewa kutokana na dhuluma za jinsia ikiwemo ukeketaji na ndoa za mapema.