SHULE YA KIBINAFSI JACK AND JILL TRANSNZOIA YANGAA KAUNTI HIYO KATIKA MTIHANI WA KCPE


Mkurugenzi wa shule ya msingi ya Jack and Jill katika kaunti ya Trans nzoia Nelson Pinto Atudo amepongeza matokeo bora ambayo yamerekodiwa na shule hiyo katika mtihani wa kitaifa KCPE mwaka 2021.
Akizungumza na wanahabari baada ya kupokea matokeo hayo ambapo mwanafunzi bora alipata alama 416, Atudo amesema kuwa wameafikia haya kutokana na juhudi za wanafunzi na walimu pamoja na ushirikiano kutoka kwa wazazi wa shule hiyo.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Roselyne Auma ambaye aidha amesema matokeo hayo yamechangiwa na hatua ya shule hiyo kukamilisha mapema silabasi licha ya changamoto zilizoletwa na janga la corona.
Wazazi wa shule hiyo wameelezea kuridhishwa na matokeo hayo ambapo wameahidi kushirikiana kikamilifu na uongozi wa shule kuhakikisha inafanya vyema hata zaidi.