SHULE NNE ZAFUNGWA BARINGO KUSINI KUFUATIA UTOVU WA USALAMA.

Wakazi kwenye baadhi ya maeneo ya Baringo kusini ambako kumeshuhudiwa utovu wa usalama wameendelea kuishi kwa hofu kufuatia kushambuliwa mara kwa mara na watu wanaoaminika kuwa wezi wa mifugo.
Uhalifu huo umesababisha kufungwa shule nne zaidi eneo hilo huku baadhi ya wakazi wakilazimika kuhamia maeneo mengine kwa hofu ya kuvamiwa.
Yanajiri haya wiki moja tu baada ya mtu mmoja kuuliwa kwa kupigwa risasi huku mifugo zaidi ya 200 wakiibwa.
Stanley kemboi mwalimu katika shule ya msingi ya kenyach aliuliwa wiki iliyopita kwenye shambulio lililomwacha babake katika hali mahututi.
Tayari shule za Kenyach, Ayatwa, Tilingwo na Chimintani zimefungwa huku sita zaidi zikitarajiwa kufungwa katika maeneo bunge ya Baringo kaskazini na kusini.