SHULE KWENYE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI ZAZINGATIA MASHARTI YA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA
Shule nyingi katika kaunti ya Pokot Magharibi zimezingatia kikamilifu masharti ya kukabili maambukizi ya virusi vya corona yaliyowekwa na serikali ili kuzuia maambukizi miongoni mwa wanafunzi.
Akizungumza baada ya kukagua miradi inayotekelezwa na serikali kuu katika kaunti hii, katibu katika wizara ya ugatuzi Mika Powon amesema ziara yao katika shule mbali mbali imebaini shule nyingi zimezingatia masharti hayo licha ya changamoto mbalimbali.
Wakati uo huo Powon amesema kufikia sasa kuna baadhi ya wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni tangu kurejelewa shughuli za masomo, akitoa wito kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanao wanarejea shuleni ili waweze kuendelea na masomo yao.