SHULE KADHAA NCHINI HAZIJAJIANDAA KUHUSIANA NA UFUNGUZI WA SHULE MAPEMA MWAKANI


Mbunge wa eneobunge la Kapenguria kaunti ya Pokot Magharibi Samwel Moroto amesema kwamba hadi sasa shule nyingi bado hazijakuwa tayari kukabiliana janga la corona kote nchini.
Akizungumza katika shule ya upili ya wasichana Holy Trinity Serewo Moroto amesema shule nyingi kaunti hii ya Pokot Magharibi hazina maji na kwamba nyingi ya shule zinalazimika kuenda mtoni ili kuteka maji.
Moroto ameshutum serkali ya kaunti ya Pokot Magharibi kwa kutowajibika vilivyo katika utengenezaji wa barabara ya kuelekea shule ya upili ya wasichana ya Serewo ikizingatiwa kwamba imelemaza shughuli nyingi.
Kando na hayo Mmoroto ameshtumu hatua ya bunge la seneti ya kumbandua mamlakani gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko katika njia ya kupiga kura kutokana na ukiukaji wa sheria kwenye uongozi wake na kusema kwamba magavana wengine wamekuwa wakipatikana kwa makosa ila hawakuwa wanachukuliwa hatua kali kama ya sonko.

[wp_radio_player]