SHUGHULI ZA MATIBABU ZATATIZIKA KACHELIBA KUFUATIA UKOSEFU WA UMEME.


Uongozi wa hospitali ya Kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi umelalamikia kukatizwa huduma za umeme katika hospitali hiyo kwa muda sasa.
Msimamizi mkuu wa hospitali hiyo Solomon Tukei amesema kuwa ukosefu wa umeme umeathiri pakubwa shughuli za kuwahudumia wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo kutafuta huduma zinazohitaji umeme.
Amesema kuwa licha ya kufahamisha mara kwa mara kampuni ya kusambaza umeme KPLC kuhusu hali hiyo hamna hatua zozote ambazo zimechukuliwa kufikia sasa.
Tukei ametaka maafisa wa kampuni ya umeme ya Kenya power kushughulikia haraka tatizo hilo ili shughuli za kawaida katika hospitali hiyo zirejelewe haraka.