SHUGHULI YA UCHIMBAJI MAFUTA TURKANA KUREJELEWA MWISHONI MWA MWAKA UJAO.


Wizara ya petroli na madini inaendeleza zoezi la kuwahusisha wananchi kuhusu mradi wa uchimbaji wa mafuta ghafi kaunti ya turkana kabla ya kurejelewa rasmi shughuli hiyo ambayo kwa sasa imesitishwa.
Akizungumza mjini Kapenguria kaunti hii ya pokot magharibi baada ya kufanya kikao na wazee pamoja na baadhi ya viongozi wa jamii ya pokot, mkurugenzi msimamizi katika wizara hiyo Elsama Ndegwa amesema wamelazimika kuwahusisha wakazi wa kaunti hii kutokana na sababu kuwa watalazimika kutumia maji kutoka bwawa la Turkwel katika shughuli ya uchimbaji mafuta hayo.
Wakati uo huo Ndegwa amesema kuwa mradi huo ambao huenda ukarejelewa mwishoni mwa mwaka ujao ulisimamishwa kutokana na mvua kubwa iliyoshuhudiwa kaunti hii ya pokot magharibi ambapo iliahithiri pakubwa hali ya barabara, pamoja na athari ambazo zilisababishwa na ujio wa janga la corona nchini.
Amekariri kuwa wananchi wote katika kaunti ya Turkana na kaunti hii ya pokot magharibi ambao wataathirika kutokana na mradi huo watafidiwa.