SHUGHULI YA KUWANUNUA MIFUGO NA KUWACHINJA YAANZA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Serkali kuu ikishirikiana na shirika la msalaba mwekundu imeanzisha mpango wa kununua mifugo na kuwachinjia Wakaazi katika kaunti kumi na tatu za maeneo kame ilikuwanusuru kutokana na athari za ukame na njaa
Akizungumza baada ya kuanza kwa shughuli ya kuwachinja mbuzi hao na vilevile kondoo kwenye kaunti ya pokot magharibi mkurugenzi katika shirika la musalaba mwekundu kaskazini mwa Kenya esther chege amesema kwamba mifugo alfu tatu na kumi watachinjwa katika kaunti ya pokot magharibi huku mifugo alfu tatu wakitarajiwa pia kuchinjwa katika kaunti ya turkana
Shughuli hiyo imefanikishwa na serkali kuu kwa kutoa ufadhili wa shilingi milioni miatano wakishirikiana na musalaba mwekundu,shirika la nyama nchini pamoja na mashirika mengine ya kijamii
Kulingana na chege watu zaidi ya laki moja na ishirini katika kaunti ya turkana wako katika hatari ya kuadhirika na baa la njaa huku zaidi ya alfu themanini na tano katika kaunti ya pokot magharibi wakiwa katika hatari io hiyo