SHIRIKA LA CY KENYA LAENDELEZA MAFUNZO SHULENI KUHUSU COVID 19.

Na Benson Aswani
Shirika la CY Kenya kwa ushirikiano na wizara ya elimu linaendeleza mafunzo katika shule mbali mbali katika kaunti hii ya Pokot Magharibi ya jinsi ya kukabiliana na visa vya maambukizi ya virusi vya corona iwapo vitaripotiwa shuleni.
Akizungumza katika shule ya msingi ya Nasokol afisa katika shirika hilo Dkt Joy Kilong Shilah amesema kuwa shirika hilo linatoa mafunzo kwa walimu wawili kutoka kamati ya kukabili maambukizi ya corona katika kila shule kaunti hii kuhusu jinsi ya kuzuia virusi hivyo shuleni.
Aidha Kilong amesema kuwa wanatumia fursa hiyo pia kuangazia hatua ambazo shule mbambali zimechukua kuhakikisha usalama wa wanafunzi shuleni dhidi ya maambukizi ya corona pamoja na changamoto ambazo zinakumbana nazo katika kutekeleza masharti ya kukabili corona.