SHINIKIZO ZATOLEWA KWA WAKUU WA USALAMA KUMCHUKULIA HATUA POLISI ALIYEMJERUHI ALIYEKUWA DIWANI TRANS NZOIA.


Shinikizo zimeendelea kutolewa kwa waziri wa maswala ya ndani ya nchi dkt Fred Matiangi, inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutiambai na mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA kumtia mbaroni afisa aliyempiga risasi na kumjeruhi aliyekuwa diwani Barnabas Lagat.
Mmoja wa wanasiasa kwenye eneo bunge la Cherang’ani kaunti ya Trans nzoia John Njuguna amelezea kushangazwa na hali kuwa afisa huyo wa kituo cha polisi cha Kapcherop katika kaunti ya Elgeyo marakwet angali huru licha ya kutumia nguvu kupita kiasi.
Diwani huyo wa zamani alipigwa risasi na polisi huyo baada yake kuingilia mvutano baina ya polisi huyo na mkazi mmoja ambaye hakuwa amevalia maski kwa kumwomba kutotumia nguvu kupita kiasi na kuwatia nguvuni wakenya wasiovaa maski.